ZAECA kuendelea na uchunguzi kwa mtuhumiwa rushwa.



Image result for zaecaMamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi  Zanzibar (ZAECA )  inaendelea kumchunguza Mtendaji wa Mamlaka ya Usimamiziwa Mazingira Zanzibar ( ZEMA ) Kisiwani Pemba  Nd. Ali Othman Mussa kwa kosa la kuomba rushwa ya shilling milioni tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Chake chake Pemba Mdhamin wa Mamlaka hiyo Pemba Nd. Suleiman Ame Juma  amesema mtuhumiwa huyo amedaiwa kuomba rushwa hiyo kwa mtu ambae jina lake lime hifadhiwa kwa kosa la kuwekewa zuiyo la kuto endelea na ujenzi katika eneo la Gombani kKisiwani Pemba.


Amesema kuwa mtuhumiwa huyo amepatikana na tuhma hizo baada ya kuskiliza malalamiko nakuandaa mtego maalum waliomnsa wakati akipokea fedha ambazio sio halali kwake kutoka kwa mlalamikaji huko ofisini kwake Machomanne siku ya jumatatu ya tarehe 31/7/2017 baada ya kupokea kiwa hicho cha fedha alicho akinadai endapo atapatiwa atamuwezesha kuendeleza na ujenzi wake ulio sitishwa.

Aidha amefahamisha kuwa sivyema kwa viongozi wa taasisi na idara mbali mbali kutumia vyeo vyao vibaya kwa kuwakandamiza walio chini kwani kufanya hivyo nikosa kisheria nao kama mamlaka husika wakilibalia watamuajibisha muhusika wa tendo hilo.

Hatahivyo amesema kuwa hilo nitukio la pili ndani ya mwezi uliopita na sasa waendelea na uchunguzi juu ya mtendaji huyo na endapo ushahidi utakamilika watamfikisha mahakani ilikujibu shutma zinazo mkabili dhidi yake ikiwa kwa sasa yupo nje kwa dhamana.

ZAECA imekuwa ikiyachukulia hatua matuo yote ya rushwa na uhujumu uchumi  kwa watendaji  mbalimbali wanao hisika na kuomba rushwa kwa kujinufaisha wao wenyewe na matumbo yao hivyo kuahidi kuzi tafutia ufumbuzi kero hizo.

Comments