Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameitaka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) kutomfukuzisha kazi kwa uzembe wao uliopelekea
nchi kupigwa na kupata hasara kutokana na watu kuingiza cement kutoka
nje ya nchi wakidai ni krinka.
Waziri
Mwijaga alisema hayo jana kupitia kipindi cha HOTMIX na ambapo alitumia
nafasi hiyo kupiga marufuku Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kukagua
krinka yoyote kutoka nje ya nchi.
"Mtu
anatengeneza Krinka anauza Kenya, sasa kama mtu anatengeneza Krinka
Tanga anauza Kenya wewe unafuata nini Pakistan? Hakuna krinka inatoka
nje ya nchi ile ni Cement iliyokamilika TRA wanashindwa kufanya kazi
yao, narudia kusema hakuna krinka inaingia nchini kutoka nje ile ni
Cement kamili na anayepinga aje aniambie mimi, na kuanzia leo TBS
wasikague krinka yoyote kutoka nje ya nchi waingize ndani ya nchi bila
TBS kukagua, TBS ipo chini yangu sasa kama mimi naambiwa sitoshi na wa
TBS ajiangalie" alisema Mwijage
Aidha Waziri Mwijage alidai kuwa watu wa Cement walikubaliana na DR Meru kununua hizo Krinka hapa hapa nchini
"Watu
wa Cement walikubaliana hapa na Dr. Meru, Twiga Cement ananunua Krinka,
Simba Cement ....mwingine nani ananunua krinka nyingine kutoka wapi,
watu wanaleta cement iliyokamilika wanasema Krinka sasa kuanzia leo TBS
hawezi kukagua krinka yoyote kutoka nje ya nchi, mpaka mamlaka iliyopo
juu yangu sasa kama TRA walizembea tukapigwa juu yao kwanini wanataka
kuniharibiana kazi, eti bwana wanataka kuniharibia kazi mimi"
alisisitiza Waziri Mwijage
chanzo:Mpekuziblog.
Comments