Waziri Maudline wa awatakaka vijana kusoma kwa bidii ili kwenda sambaba na soko la ajira.

Maudline
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico  amewataka vijana  nchini  kusoma kwa bidii ili kwenda sambamba na soko la ajira lenye kutaka vijana wenye elimu, ujuzi na uzoefu.

Akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa mafunzo ya uwanajenzi  kwa  vijana wa chuo cha utalii amesema kutokana na hali ngumu katika soko la ajira lazima kuwepo kwa  watendaji  wenye nguvu kazi kielimu na sifa zenye kukubalika  katika soko la ajira.

Amesema katika soko la ajira  wafanyakazi  ni wajibu wao  kutoa huduma bora kulingana na elimu pamoja na ujuzi walio nao  na waajiri  kutoa ajira  ambapo amesema kiwango cha kazi  hupimwa  kutokana na  elimu, ujuzi na uzoefu walionao vijana.
Hata hivyo amesema  endepo vijana watakuwa na mazingira bora katika soko la ajira  wataweza  kutengeneza  uchumi  wa taasisi  na taifa  kwa maendeleo endelevu.
Aidha castico amesema licha ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali duniani kuhakikisha vijana  wanakwamuka na tatizo la ajira bado kuna changamoto za muda mrefu  kwa waajiri Zanzibar  wamekuwa na kilio  kwamba vijana  wengi waliopo  katika soko la ajira  hawana sifa stahiki zinazohitajika katika soko  na kuwa na wasiwasi na uimara  katika taasisi zao.
Amefafanua miongoni mwa mapungufu  hayo ni pamoja na elimu duni kwa vijana,kiwango  kidogo  cha ujuzi na uzoefu  katika fani mbalimbali  ambapo matokeo yake waajiri  hutafuta  wafanyakazi wa kigeni  ili  kuziba upungufu katika taasisi zao.
“kutokana na kasoro mbalimbali zinazotajwa na waajiri lazima nitapambana kuhakikisha vijana wa Zanzibar   wanasoma  na kupata ujuzi wa fani mbalimbali  ili kuuzika katika soko la ajira na kwa hawa vijana walioingia katika mafunzo haya ya uwanajenzi wataandaliwa  vyema ili kuondoa kasoro zilizopo”amesema Castico.
Kwaupande wake Mwakilishi kutoka shirika la kazi duniani ILO Ashwani Aggrwal amesema  kutokana na  umuhimu wa ajira nchini shirika la kazi limekuwa likiweka  mikakati na misaada ya kitaalamu  na fedha kuzisaidia  nchi mbalimbali  duniani  ili kukuza  ujuzi  kwa vijana ikiwa lengo ni  kuwepo kwa sifa stahiki katika soko la ajira ili vijana kuweza kujiajiri wenyewe na hata kuajiriwa.
Hata hivyo ameeleza  kuwa Programu hiyo ya mafunzo kwa vijana ni miongoni mwa hatua za kuwajengea mazingira bora  vijana  na kuwajengea daraja  madhubuti katika  ulimwengu wa kazi  na mafunzo ili kuwepo kwa uwiyano mzuri baina ya ujizi na mahitaji ya soko au taasisi nchini.
“Tutadumisha ushirikiano wetu  na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika kuwajenga  vijana mbalimbali duniani ili wende sambamba na soko  na lengo letu hasa ni  kupunguza wimbi la vijana walio mitaani  kuweza kujiajira kwa fani mbalimbali hata za ujasiriamali”
Nae Mkurugenzi kutoka chuo cha utalii Zanzibar SUZA Aley Soud Nassor ametoa wito kwa  serikali pamoja na shirika la kazi duniani  kuwa bega kwa bega na walengwa wa mafunzo hayo ili fursa hiyo iweze kudumu na kuweza kuwafikia walengwa waliokusudiwa ili  kuweza kunufaika  na program hiyo.
Wakati huo huo Mwanafunzi kutoka chuo cha utalii aliyekuwepo katika program ya mafunzo hayo ya uwanajenzi Asia Salum Omar  akisoma risala ya wanafunzi amesema wamefarajika na ujio wa mafunzo ambayo yatawajenga ili kuingia katika soko la ushindani ili kupata ajira lakini amesema tatizo kubwa linalowakabili  wanapokwenda kufanyakazi kwa vitendo katika mahoteli kutoruhusiwa kuvaa mitandio  kwa wanawake  jambo waliloomba kutafutiwa ufumbuzi  na serikali kuliingilia kati ili kuweze kudumishwa kwa mavazi ya kizanzibar katika sehemu za kitalii.
Aidha ameitaka serikali kwa kushirikiana na wadhamini  kuwaendeleza  vijana kielimu zaidi  kutoka  ngazi ya cheti hadi kufikia Digrii.
“Tunaamini utalii wetu wa Zanzibar utaendana na historia yetu  kwani tusidumishe  mavazi yetu ili twende sambamba na  mila na desturi zetu kama wanavyofanya  mataifa mengine duniani kudumisha  mazehebu yao kwa mavazi”
chanzo:Zanzibar24

Comments