Watanzania wametakiwa kutumia mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta.

Watanzania na wadau wa kutoa huduma ya sekta ya mafuta na gesi nchini wametakiwa kutumia fursa ya uwekezaji katika mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi unaotarajiwa kujengwa kutoka Tanzania hadi uganda .

hayo yameelezwa na mwanzilishi mwenza na makamu mwenyekiti wa jumuiya ya watoa huduma ya mafuta na gesi (atogs) ndugu abdulsamad abdrurahim wakati akizungumza na wandishi wa habari katika hoteli ya serena jijini Dar es salam ambapo ameelezea namna serikali ya tanzania ilivyoonyesha utayari katika kushirikiana na sekta binafsi katika utekelezaji wa mradi huo.


nae katibu mkuu wa wizara ya nisharti na madini dr. juliana pallangayo amesema sera ya taifa ya nisharti inahamasisha ushirikishwaji wa wadau wa sekta ya mafuta gesi hivyo amewataka watanzania kutumia fursa hiyo ilikuweza kunufaika kiuchumi.

mapema nae kurugenzi wa baraza la taifa la uwezeshaji kiuchumi Nd. Edwin Chrisount amesema baraza litahakikisha linasimamia ipasavyo sheria ya uwekezaji ili mradi huo kufaidisha jamii ya watanzania.

jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi tanzania linataraji kuwekwa na marais wa tanzania na Uganda Mhe Dkt John Pombe Magufuli na Yoweri Kaguta Museveni tarehe 05/08/2017 ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu.
chanzo:Zbc.

Comments