Mwenyekiti
wa Kamati ya uchaguzi mkuu wa TFF Revocatus Kuuli amemtangaza Wallace
Karia kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufuatia
uchaguzi wa shirikisho hilo uliofanyika jana Makao Makuu ya Tanzania
Dodoma.
Wallace
Karia aliibuka mshindi wa nafasi ya Urais wa shirikisho hilo huku
nafasi ya Makamu ya Rais ikichukuliwa na Michael Wambura,.
Kwa matokeo hayo Wallice Karia anakuwa mrithi wa aliyekuwa Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Jamal Malinzi
Baada
ya kutangazwa washindi viongozi hao waliweza kula kiapo mbele ya
wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi, na baada ya hapo Rais mpya wa shirikisho
la mpira wa miguu (TFF) Wallace Karia aliwashukuru wajumbe na watanzania
kIujumla na kusema kuwa furaha aliyonayo iende kuwa furaha ya kazi kwa
kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya soka la Tanzania.
Hata
hivyo Wallace alisema katika uongozi wake uwazi na uwajibikaji ndiyo
nguzo kuu na kusema hivi sasa ubabaishaji katika mpira wa miguu sasa
umekwisha, ubabaishaji wa soka sasa ni mwisho.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments