Mahakama
Kuu ya Tanzania inatarajia kutoa uamuzi wa ama kuyasikiliza au
kutoyasikiliza maombi ya Wabunge 8 wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi
CUF waliofutiwa uanachama na Mwenyekiti Prof. Lipumba ifikapo August 4,
2017.
Hatua
hiyo imetokana na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata kuwasilisha
pingamizi la awali mbele ya Jaji Lugano Mwandambo akipinga kufunguliwa
kwa kesi hiyo.
Malata
ambaye anashirikiana na Mawakili wengine Tisa alimueleza Jaji Mwandambo
kuwa anapinga maombi hayo kwa kuwa yamefunguliwa kwa njia isiyo sahihi
akisema yamefunguliwa bila kuwekwa kifungu sahihi kinachoipa Mahakama
mamlaka ya kusikiliza na kutoa uamuzi dhidi ya maombi hayo.
Aidha,
amedai maombi hayo yamefunguliwa chini ya kifungu kidogo cha 2(3)
ambacho kinaipa mamlaka Mahakama kutumia sheria ya Jumuiya ya Madola.
”Kama
maombi hayo yameletwa chini ya kifungu hicho ilipaswa kiwepo kifungu
husika kutoka katika sheria ya Jumuiya ya Madola, kisheria kinapaswa
kutumika endapo hakutakuwa na sheria yeyote Tanzania inayozungumzia
maombi hayo”.Amesema Malata
Malata amedai maombi hayo ni batili, hivyo yatupiliwe mbali kwani hata Mahakama iliwahi kutoa uamuzi dhidi ya kifungu hicho.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments