Vijiji 11 vyapatiwa fedha kutokana na uhifadhi.

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Enduimet (WMA) imekabidhi Sh99 milioni kwa vijiji 11 wilayani Longido kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya wananchi.
Fedha hizo zimetolewa na kampuni ya uwindaji ya Shangri-la iliyopo wilayani Longido mkoani Arusha.

Imeelezwa kuwa fedha hizo zinatokana na mapato yaliyokusanywa kwa ajili ya shughuli za uwindaji katika kampuni hiyo.
Vijiji hivyo 11 vinavyounda jumuiya hiyo kwa kutoa maeneo ya shughuli za uwindaji  kila kimoja kimepewa Sh9 milioni.
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo amewaagiza watendaji wa vijiji husika kuhakikisha wanaainisha mapato na matumizi ya fedha hizo katika kila kijiji ili zijulikane zilivyotumika.
Chongolo amesema kumekuwepo ubadhirifu wa fedha za wananchi unaofanywa na watendaji wanaojali masilahi binafsi ikiwemo kujilipa posho.
chanzo:Mwananchi.

Comments