
Mkuu wa wilaya ya wete Rashid Hadidi Rashid amesema si ruhusa kwa Mwananchi yoyote kununua ama kuuza karafuu kwa njia ya kikombe na atakae kwenda kinyume hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na wanunuzi ama wauzaji wa karafuu kwa njia ya kikombe huko ofisini kwake wete.
Amesema ununuzi wa karafuu kwa njia ya vikombe kunachangia wizi wa karafuu hivyo ameeleza kuwa mtu yoyote ambae atakamatwa akinunua ama kuuza karafuu hatua za kisheria zituchukuliwa dhidi yao.
Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi kutouza karafuu zao majumbani na badala yake waziuze karafuu zao katika vituo vya ZSTC ili serekali iweze kujipatia mapato kupitia zao hilo.
Na OCD wilaya ya wete Hamad Omar Sleiman amesema kumejitokeza baadhi ya watu huchukua karafuu kutoka tanga kwa njia ya magendo na kuzichanganya na karafuu za pemba jambo ambalo linapelekea karafuu za pemba kuzipotezea sifa yake hivyo mtu yoyote atakae kamatwa hatua za kisheria zitachukuliwa.
Kwa upande wa Wananchi wameahidi kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya na kuhakikisha kwamba wanaufikisha ujumbe huo kwa wananchi wengine.
chanzo:zanzibar24.
Comments