
Afisa mwandamizi katika upinzani huo James Orengo amesisitiza kuwa hawatakwenda mahakamani ili kuafikia lengo lao.
Amewataka wafuasi wao kuwa watulivu na kujilinda dhidi ya 'madhara' ya serikali.
Bwana
Orengo amedai kwamba takriban watu 100 ikiwemo watoto wameuawa na
vikosi vya usalama vya Kenya huku miili yao ikitiwa ndani ya mifuko ya
plastiki.
Alionyesha vibweta vya risasi lakini akashindwa kutoa ushahidi kuthibitisha madai hayo.
Matokeo rasmi yalionyesha kuwa rais Uhuru kenyatta alipata
asilimia 54.3 ya kura huku mpinzani wake mkuu Raila Odinga akitaja
matokeo hayo kama ''mchezo mkubwa''.
''Walijua kwamba wataiba kura
.Walijua kwamba watu hawatafurahia kwa hivyo vifaa vyote vya
kukabiliana na ghasia viliwekwa tayari'', alisema Orengo.
Huku
ikiwa waandishi hawajaona ushahidi wa kuthibitisha mauaji hayo
yanayodaiwa na upinzani, takriban watu 11 wameripotiwa kuuawa na polisi
katika maeneo yanayomuunga mkono Raila Odinga.

Chumba cha kuhifadhi maiti cha kaunti ya Nairobi kilipokea miili minane.
Kenya Fred Matiangi aliwataka Wakenya kurudi katika maisha yao ya
kawaida na kuwataka wale wanaotumia mitandao ya kijamii kuitumia vizuri.
Rais Kenyatta ameomba kuwepo na amani.
''Tumeona
matokeo ya ghasia za baada ya uchaguzi , Najua kwamba hakuna Mkenya
mwengine ambaye angependa kurudi katika ghasia hizo'', alisema.
Kabla
ya matokeo hayo kutangazwa bwana Raila Odinga aliwaomba wafuasi wake
kuwa watulivu, lakini akongezea kuwa hawezi kumdhibiti mtu yeyote na
kwamba watu wanataka kuona haki.
Shirika la haki za kibinaadamu la Amnesty International limeitaka serikali kuchunguza mauaji hayo.
chanzo:Bbc.
Comments