
Kiongozi mmoja mkuu wa chama cha upinzani, Bwana Johnson
Muthama, amesema kuwa polisi wanajaribu kuwalazimisha watu "wakubali
matokeo hayo."
Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya, ambao ulishindwa katika uchaguzi
mkuu wa mwaka huu, umeapa kuendelea na maandamano wenye nia ya
kubatilisha kile ambacho unasema kuwa, matokeo "feki" ya uchaguzi mkuu.
Mpinzani mkuu wa Bw Kenyatta, Bw Raila Odinga, amedai kuwa uchaguzi huo ulikubwa na wizi mkubwa wa kura.
Seneta James Orengo ameiambia BBC kuwa chama chake,
kinachoongozwa na Bw Raila Odinga, hakitapinga matokeo ya uchaguzi mkuu
mahakamani, huku akisema kuwa Uhuru Kenyatta tayari ametoa vitisho kwa
majaji.
Tume
ya taifa ya kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya, imetoa orodha ya
juu ya wahasiriwa wa ghasia hizo huku ikisema kuwa ni watu 24 ndio ambao
wameuwawa katika visa vinavyohusiwa na uchaguzi huo, huku ikiongeza
kuwa polisi wanatumia nguvu kupita kiasi.
Kaimu Waziri wa usalama wa ndani, Fred Matiangi, amewataja waandamanaji kama "wahalifu".
chanzo:Bbc.
Comments