Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein amesema mpango kazi wa kitaifa wa kumaliza ukatili na udhalilishaji Zanzibar ni azma ya serikali ya mda mrefu yakutaka kuirejesha hadhi ya mwanamke na mtoto katika jamii.
![]() |
Waziri wa kazi Uwezeshaji,wazee,vijana,wanawake na watoto Maudline Cyrus Castico akitembelea maonyesho mbalimbali yaliyoandaliwa na asasi za kiraia kudhibiti vitendo vya ukatili naudhalilishaji wanawake na watoto Zanzibar.. |
Akizindua mpango huo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Waziri wa kazi Uwezeshaji,wazee,vijana,wanawake na watoto Maudline Cyrus Castico amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imezindua mpango kazi huo utakaofanyakazi kwa muda wa miaka mitano, utategemea kumaliza ukatili na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto Zanzibar.
Amesema mpango huo umeweka mikakati imara ya kuvidhibiti vitendo vya ukatili na udhalilishaji visiweze kutokea Zanzibar na endapo vikitokea mpango huo uweze kufanya kazi kiuadilifu.
![]() |
Wakuu wa mikoa pamoja na wakuu wa wilaya na viongozi mbalimbali wakifuatilia maadhimisho ya mpango kazi wa kudhibiti vitendo vya ukatili na udhalilishaji wanawake na watoto Zanzibar. |
Kwaupande wake mtoto Jaffar Ahmada akisoma risala kwa niaba ya watoto wa Zanzibar amesema vitendo vya ukatili na udhalilishaji wanavyofanyiwa na jamiii inayowazunguka vimekuwa vinawarudisha nyuma na kuwaumiza kisaikolojia kama vile kupigwa,kulawitia,kuchomwamoto pamoja na vichanga kutupwa.
Aidha wameitaka serikali kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa pamoja na wadau wa maendeleo nchini kuchukua hatua madhubuti zitakazotumika katika mpango huo wa miaka mitano kutoa adhabu kali kwa wataohusika na vitendo vya kuwadhalilisha watoto.
Wakati huo huo Fatma Abdalla Mussa akisoma risala ya wanawake wa Zanzibar ameitaka serikali kuyafanyia kazi na kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya udhalilishaji yanayowakumba wanawake kama vile kutelekezwa na watoto,kupigwa,kubakwa, kunyimwa haki ya kurithi pindi wanapoachika katika ndoa pamoja na kuondoa wimbi la talaka katika jamii.
Amesema endapo mpango huo utafanya kazi kwa uwadilifu na kufuata sheria utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa kilio na maumivu ya muda mrefu katika mioyo ya wananchi.
Nae Katibu mkuu wizara yakazi,uwezeshaji,wazee,vijana,wanawake na watoto Fatma Harib Bilali amesema mpango huo umezingatia sera na sheria za udhalilishaji, kuimarisha mila na desturi za wananchi kuweka mazingira salama, kuwawezeasha wanawake kiuchumi,kuweka mifumo mizuri katika vyombo vya sheria kuhakikisha vitendo hivyo vinamalizika
Amesema kuzinduliwa kwa mpango huo utaweza kutela faraja na kuzaa matunda kwa jamii na serikali na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwaongoza vyema watoto katika malezi bora.
Kwaupande wa wizara mbalimbali za serikali ikiwemo wizara ya katiba na sheria,Wizara ya tawala za mikoa na idara maalum,Wizara ya Afya,Wizara ya elimu,Wizara ya habari Zanzibar zimeahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika kupambana kila mmoja kwa nafasi yake ili kuuwezesha mpango huo kufanya kazi ya kumaliza ukatili na udhalilishaji visiwani Zanzibar pamoja na kuzifanyia marekebisho ya baadhi ya sheria zilizokuwa na matatizo ambazo hukwambia kesi kushindwa kuendelea mbele.
Mapema Jeshi la Polisi limetoa ahadi ya Kuongeza kasi ya upelelezi wa kesi kwakushirikiana na Ofisi ya DPP ili kutoa msukumu wa kurahisisha ufatiliaji wa kesi hizo za ukatili na udhalilishaji na kuisaidia mahakama kuweza kutoa adhabu kali ili kuwa fundisho kwa wahalifu.
![]() |
Askari wa Jeshi la Polisi wasikiliza kwa umakini zaidi Hotuba ya Rais wa Zanzibabar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Ali Muhammed Shein iliosomwa na Waziri wa kazi Uwezeshaji,wazee,vijana,wanawake na watoto Maudline Cyrus Castico. |
Uzinduzi huo uliowakutanisha watu zaidi ya mia nne asasi za kiraia,mashirika ya kimataifa,jeshi la polisi watendaji wa mawizara,taasisi za kidini.
chanzo:Zanzibar24
Comments