Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Bi Mwanajuma Majid Adalla amewataka Masheha na Madiwani Mkoani kuwa na mashirikiano ya pamajo na mabaraza ya Vijana ili kuhakikisha lile lengo la kuundwa mabaraza hayo linafikiwa.
Wito huo ameutoa katika mkutano wa Masheha Madiwani pamoja na baraza ya miji Mkoani kwenye ukumbi wa skuliya maendeleo Mkwachani katika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji wa sera kwa vijana wa mkoani uliofadhiliwa na the foundation for Civil Society lengo la Serekali kuanzisha mabaraza ya Vijana ni kuwakusanya pamojo ili kuweza kutatua changamoto zao zinazowakabili.
Kwa upande wake mkuu wa Idara ya vijana pemba kutoka Wizara ya kazi Ustawi wa Jamii Vijana Wazee Wanawake na Watoto amesema vijana wana mchango mkubwa wa kuendeleza maendeleo ya kiuchumi katika nchi kwani ndio nguvu kazi ya taifa
Amesema kuna haja ya kuendelezwa vijana katika kiuchumui kwani ndio tegemezi la taifa katika kuleta maendeleo nchini na mwenyekiti wa baraza la vija wa wilaya ya mkoani ali said ali amesema mabaraza ya vijana tayari yameshaleta matumaini wilaya ya mkoani katika shehia tano kwa uzalishaji wa kilimo cha boga bonga na sasa kuwahimiza vijana hao kujiendeleza ili kujikwamuwa na umasikini.
Baahdi ya washiriki wa mkutano huo wamezitaka asasi na jumuiya pamoja na serekali kuwajengea uwezo vijna kuwawezesha katika kuwapatia elimu ya ujasiriamali ili kujikimu kimaisha na kuwacha kusubiri ajira kutoka Serekalini.
Katika mradi huo wa kuboresha utekelezaji wa kuboresha sera za vijana ambapo kauli mbiyu ni kijana paza sautio changamkia fursa.
chanzo:zanzibar24.
Comments