SMZ yajipanga kupambana na ajali za baharini.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Abdalllah Hussen Kombo amesema  kutokana na wananchi kuwa na mwamko mkubwa wa kutumia Usafiri wa anga na Baharini Serikali inaendelea na utaratibu wa kuimarisha usafiri huo ili kuweza kulinda usalama wa Wananchi na mali zao wakati wa safari.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya miundombinu na usafirishaji, katika mkutano wa kuwaelimisha wadau wa sekta ya uchukuzi juu ya mpango wa Taifa wa utafutaji na Uokozi (SEARCH AND RESCUE PLAN) mkurugenzi huyo amesema watendaji wa Mamlaka za usafiri watakapofanya kazi kwa Bidii na sheria watasaidi kupunguza ajali zinazojitokeza.


Amesema kuna Ajali Nyingi zimejitokeza na kusababisha majanga makubwa kwa wananchi na hasara kwa serikali ikiwemo kuzama kwa meli, hivyo Serikali ya Zanzibar imekusudia kuweka boti tatu zitakazorahisisha huduma za Uokozi kwa wakati, katika maeneo ya Bandari ya Mkokotoni Unguja ,Mkoani pamoja na Wete Pemba.

Kwa upande wao washiriki wa Mafunzo hayo Wameziomba Serikali za Tanzania kuimarisha mawasiliano ya Vyombo vya Baharini ili watumiaji wa vyombo hivyo waweze kutoa taarifa kwa wakati wakati wanapokutwa na majanga wakiwa safarini.

Wamesema majanga mingi yanatokea wakati wanapokuwa safarini na kushindwa kuripotiwa kwa wakati kutokana na kukusekana kwa mawasiliano ya uhakika jambo ambalo hupelekea vifo kwa wasafiri na upotevu wa mali.

Nae kaimu mkurugenzi wa Usalama na mazingira katika wizara ya ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano ya Muungano Stela Joshua Katondo ,amesema kutokana na kuchelewa kwa taarifa za majanga ya Anga na baharini mafunzo haya yatasaidi upatikana wa taarifa kwa haraka ili waweze kuwaokoa wasafiri wanapopata matatizo wakiwa safarini.

Amesema mafunzo hayo pia yanaendelewa kutolewa kwa nchi zote za Africa mashariki ili kuongeza ushirikiano wa uokozi katika nchi hizo, pamoja na kuwatambua wasafiri watakaopata majanga kupatiwa huduma muhimu ikiwemo waliofariki kufikishwa kwa familia zao.

Aidha amesema pindipo mpango huo utakamilika utaonesha namna bora na salama ya uokoaji kwa wasafiri ili waweze kuokoa mali za na maisha wa watu bila kusababisha upotezo wa rasilimali hizo.

Mafunzo hayo ya siku moja yametowa kwa watendaji wa Mamlaka za Anga na Usafiri wa Baharini ,watendaji wa Jeshi la Polisi ,Wavuvi ,wizara zinahusiana na uokozi na uchukuzi pamoja na baadhi ya Viongozi wa wilaya na mikoa ili waweze kupambana na majanga yanayoweza kujitokeza katika maeneo yao ya kazi.

chanzo:Zanzibar24.

Comments