
Zanzibar24 ilifunga safari hadi tume ya utangazaji Zanzibar na
kukutana na Mhandisi wa tume hiyo Ali Hussen Ayoub kufahamu undani wa
jambo hilo.
Mhandisi aliiyambia zanzibar24 kuwa Zanzibar itazima mitambo yake ya
Analogi ifikapo tarehe 31 na kuwasha Digital licha ya kuwa wamechelewa
kwa muda mrefu kulikosababishwa na maboreshe mbalimbali ya mitambo na
mambo mengine.
Amesema ujio wa mitambo mipya ya digital imekuja baada ya makubaliano
ya nchi wanachama wa jumuiya ya mawasiliano ya umoja wa mataifa (ITU)
kwamba nchi wanachama wote wabadilishe mifumo yao ya kurusha matangazo
ya televisheni kutoka analogi kwenda digitali ili kuboresha huduma kwa
wananchi.
Aidha amesema mifumo ya digitali itaweza kuleta faraja na maendeleo
makubwa kwa wananchi wa Zanzibar kwa kupata huduma zenye ubora na
uhakika ambapo kutapungua gharama za uwendeshaji na kuwataka wananchi
kutoa ushirikiano kwa serikali kwani jambo hlilo litaweza kuleta
maendeleo.
Hata hivyo amesema bila ya kupata maendelo ya mifumo ya utangazaji
Zanzibar haitaweza kuendelea hivyo wananchi lazima wakubaliane na
mabadiliko hayo yenye faida kwani kutaongezeka kwa chanal
mbalimbali pamoja na kuongezeka vituo vya televition visiwani Zanzibar
na kuweza kupata wataalamu wazuri.
Muhandisi wa tume hiyo amewataka wananchi wa Zanzibar kununua
vin’gamuzi ili kupata urahisi na ubora wa hali ya juu na kupata chanali
tofauti na bila ya kununua kin’gamuzi hawataweza kuonana kitu katika
tv zao.
Amesema wakiwasha mitambo ya digitali tarehe 31 kwa wananchi na
mashirika wanaotumia analogi hadi leo hawataona kitu na vifaa vyao
vitazima hivyo nivyema wakatafuta njia mbadala mapema ili kwenda
sambamba na nchi zilizoendelea.
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya mji wa Zanzibar wametoa maoni yao
juu ya ujio wa mitambo mipya ya digital wamesema ni jambo zuri lakini
kutokana na hali duni za wananchi watashindwa kumudu gharama za mitambo
hiyo.
Wamesema lazima serikali iyangalie hali ya uchumi ya wananchi wake kabla ya kuanza kwa mitambo hio ya digitali.
“Nijambo zuri la digitali lakini sisi wananchi hasa wa vijijini
inatushinda pesa ya chakula tutaweza kumudu gharama za digital ipo haja
serikali ikapunguza gharama za manunuzi ya vin’gamuzi pamoja na ada ya
kila.
chanzo:Zanzibar24
Comments