Katika
jitihada za kuwadhibiti wafanyabiashara wa mashamba makubwa
wanaoyatumia kwa ajili ya kukopea fedha na kisha kutoyaendeleza,
serikali inatarajia kuanzia mwakani, kuwasilisha bungeni Muswada wa
Marekebisho ya Sheria ya Ardhi, utakaowadhibiti wafanyabiashara hao.
Hatua
hiyo, imetokana na namna Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, ilivyobaini uwepo wa mashamba mengi yakiwemo yanayomilikiwa na
wafanyabiashara wakubwa nchini ambayo hayajaendelezwa huku yakiwa
yamekopewa fedha nyingi na kutumika katika biashara nyingine.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Moses
Kusiluka amesema sheria hiyo italenga kudhibiti watu kutumia mashamba
kujipatia fedha na kisha kuyatelekeza.
“Tunataka
kupitia sheria hii, mtu akikopa kupitia mashamba haya, fedha hizo
zitumike kuyaendeleza na siyo kuyaacha mapori na kufanya biashara zake
nyingine. Sheria itaweka masharti kuwa mikopo yote yenye dhamana ya
mashamba, isimamiwe na benki zenyewe,” alisema.
Alisema
katika mpango unaoendelea wa kushirikiana na halmashauri za wilaya
kufanya ukaguzi wa mashamba yasiyoendelezwa wamebaini mashamba mengi
ambayo hayajaendelezwa yakiwemo yaliyochukulia mikopo benki.
“Mashamba
yote yasiyoendelezwa baada ya kufuata taratibu zote, ikiwemo kutoa
notisi kwa wamiliki tumeyawasilisha kwa Rais John Magufuli kwa ajili ya
kubadilishiwa umiliki.Haya yaliyochukulia mikopo, sheria inaturuhusu
kuyataifisha pia,” alisema.
Hata
hivyo, alisema mashamba hayo yaliyochukulia mikopo kwa sasa
wanazungumza na benki husika ili kuangalia namna ya wahusika wa mashamba
hayo kubadili dhamana za mikopo yao ili yaweze kurejeshwa mikononi mwa
serikali.
“Tunafanya
hivi si kwa sababu eti hatuna uwezo wa kuyachukua la hasha, tunafanya
hivi ili kunusuru benki hizi, kwani mashamba mengi yamechukulia mikopo
mikubwa endapo tutayataifisha na kuyachukua kama hakuna dhamana nyingin"
chanzo:Mpekuziblog.
Comments