Serikali ya Korea yaahidi kusaidia ujenzi wa miundo mbinu ya kilimo cha umwagiliaji maji, mkoa wa kaskazini pemba.

Image result for pemba islandSerikali ya Jamhuri ya watu wa Korea imeahidi kusaidia ujenzi wa miundo mbinu ya kilimo cha umwagiliaji maji, kwa kuimarisha kilimo cha mpunga  kwa wakulima wa mkoa wa kaskazini pemba .

Balozi wa jamhuri ya watu wa korea hapa nchini  song geum young, alisema kuwa, kuimarishwa kwa miundo mbinu hiyo itasaidia kuongeza uzalishaji wa mpunga kwa wakulima  .


Akizungumza na katibu tawala mkoa wa kaskazini Pemba, huko afisini kwake, Mnazi mmoja Wete, balozi song geum young  alisema, mafanikio yanaweza kupatikana na kufikia maendeleo yaliokusudiwa, iwapo kutakuwa na ushirikiano wa wananchi wa Pemba hususani maeneo ambayo miradi hiyo itatekelezwa.

‘’Ushairikiano ni muhimu ,wananchi wawe na muamko na kuunga mkono misaada inayowafikia katika kuendeleza kilimo’’, balozi young alisema.

Sambamba na hayo, alisema kuwa Serikali hiyo, imelenga kusaidia katika sekta ya elimu kwa kuchangia madawati, ili kupunguza tatizo la vikalio maskulini.

Naye  Katibu Tawala Mkoa wa kaskazini Pemba, Ahmed Khalid Abdalla, alisema serikali ya mapinduzi ya zanzibar imekuwa ikichukua hatua za makusudi kuimarisha sekta ya kilimo, ili kuwawezesha wakulima kuzalisha chakula cha kutosha.

‘’Tunashukuru na tutashirikiana nanyi kuona kuwa malengo yanafikiwa kwa kuwasaidia wananchi katika Sekta hii ya kilimo, na kuona kuwa wanajikimu kwa chakula’’, Katibu Tawala alieleza.

Aidha amesema serikali ya mkoa itashirikiana na serikali ya jamhuri ya watu wa korea, ili kuona kwamba utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo unakamilika na kuleta tija kwa wananchi .

Hata hivyo katibu tawala ameitaka serikali ya jamhuri ya watu wa korea kusaidia kuyatangaza maeneo ya utalii  yaliyopo Zanzibar, ili watalii waweze kutembelea visiwani jambo ambalo litachangia kupatikana kwa pato la taifa.

Jumla ya dola za kimarekani milioni kumi zinatatarajiwa kutumika katika kusaidia miundo mbinu ya kilimo cha umwagiliaji maji kutoka katika ufadhili wa Serikali ya watu wa Korea.

Comments