Serikali inaandaa mpango mbadala wa kuondoa matumizi ya nishati ya mkaa.

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira mh. January makamba amesema serikali inaandaa mpango mbadala wa kuondoa matumizi ya nishati matumizi ya mkaa na kuni iili kukabiliana na athari kubwa ya uharibifu wa mazingira tanzania.

Mh. Makamba ametowa tamko hilo afisini kwake dar esalaam ambapo amesema kutokana na mahitaji makubwa ya matumizi ya mkaa nchini ambayo yamekuwa yakileta athari ya mazingira kwa kupitia wizara yake tayari imeshaandaa warsha ya wadau mbali mbali kwa lengo la kujadili na kushauriana kutafuta mbinu endelevu za kupunguza matumizi ya nishati hiyo.


Aidha mh. Makamba amefahamisha kuwa ripoti ya pili ya hali ya mazingira nchini iliyochapishwa mwaka 2014 imebainisha hali mazingira nchini si ya kuridhisha na kuonyesha kasi ya uharibifu wa misitu ni kubwa ambapo kila mwaka zaidi ya hekta laki tatu zinaangamizwa licha ya serikali na wadau wengine kuwa na mipango mingi mizuri.

Hata hivyo amesema zaidi ya asilimia 90 ya watanzania nchini wanatumia mkaa na kuni kama ni nisharti ya kupikia na mwanga ambapo serikali ni moja ya mtumiaji mkubwa wa kuni na mkaa kupitia tasisi za umma ikiwemo mashule,magereza ,vyuo,na kambi za majeshi.

Amesema tayari wizara yake imeshafanya vikao na wadau mbalimbali na jumuiya za wazalishaji na wasambazaji wa gesi ya kupikia nchini kufunga mitambo ya kuhifidhia gesi na majiko ya gesi katika taasisi za serikali pamoja na kupunguza gharama za ununuzi wa nishati hiyo. 
chanzo:Zbc.

Comments