
Zoezi hilo limesimamiwa na Kaimu Afisa Elimu wa Manispaa ya
Kigamboni, Mwalimu Mathew Komba pamoja na Wakaguzi wa Elimu katika
manispaa hiyo ambapo mapungufu mbalimbali waliyabaini kama shule
kutokuwa na usajili, madarasa machache, kutokuwa na vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu n.k.
Katika siku ya kwanza ya ukaguzi huo, timu hiyo imezifunga shule 18
kati ya 58 zilizobainishwa kutokuwa na usajili katika kata za Kigamboni,
Vijibweni na Tungu.
Miongoni mwa shule zilizofungwa ni Malaika Nursery School, Kigamboni
English Medium School, Patmos, Montecarlos, Riziki, Taqwa, Firdaus na
Meck.
Hata hivyo, uongozi wa Manispaa ya Kigamboni imewataka wazazi
kutowapeleka watoto wao kwenye shule hizo mpaka hapo watakapokamilisha
taratibu walizowekewa ikiwemo kupata usajili.
chanzo: zanzibar24.
Comments