Mh. Riziki ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na walimu
na watendaji wa vituo vya mafunzo ya amali kwa kuwataka
watekeleze vyema dhamana walizopewa kila mmoja kwa nafasi yake
pamoja na kuwa wabunifu katika kuitumia mitaala wanyofundishia.
Wakielezea matatizo yanayowakwaza katika kutekeleza kazi zao
wafanyakazi hao wamesema ni pamoja na maslahi duni,uhaba wa
vifaa vya kufundishia ikiwemo computer,na ukosefu wa huduma ya
bima ya afya ambayo ni muhimu kutokana na vitendea kazi
hatarishi wanavyotumia.
Katika hatua nyengine mh.riziki amekabidhi hundi ya shillingi
million tano kwa kikundi kinachojishughulisha na ufundi wa
komputer kiliopo mwanakwerekwe ambacho ni matunda ya vituo hivyo.
Mkurugenzi mtendaji mamlaka ya mafunzo ya amali bakar ali
silima amesema tayari wameshatumia shillingi millioni khamsini
kwaajili ya kuvipatia mkopo vikundi kumi vinavyotokana na
vyuo hivyo.
chanzo:Zbc.
Comments