Jeshi
la Polisi limemaliza zoezi la kufanya upekuzi katika nyumba ya
Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyopo
Tegeta Dar es Salaam na baada ya hapo Lissu amerejeshwa Kituo Kikuu cha
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Jeshi
la polisi lilikwenda nyumbani kwa Tundu Lissu kufanya ukaguzi kufuatia
makosa mawili ambayo Mbunge huyo wa Singida Mashariki na Rais wa TLS
anatuhumiwa nayo ambayo ni pamoja na Kusema makosa ya Rais John Pombe
Magufuli hadharani na chochezi kuhusu kushikiliwa ndege ya Tanzania aina
ya Bombardier Q400 huko nchini Canada.
Kwa
mujibu wa Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene amedai kuwa Tundu
Lissu amerudishwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya taratibu zingine
za kisheria ambazo zitaendelea ikiwa pamoja na dhamani ambayo kisheria
ipo wazi.
Tundu
Lissu alikamatwa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2017 na jeshi la polisi
alipotoka mahakamani kwenye kesi ya uchochezi , alipelekwa Police
Central kwa ajili ya kufanyiwa mahijiano na baadaye kulala rumande
kutokana na jana kushindwa kupewa dhamana.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments