Mashirika ya kimataifa yamethibitisha kuwa uchumi wa tanzania unakuwa kwa kasi.

Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo dr. Hassan abass amesema mageuzi makubwa yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano yamesaidia nchi kuwa na uchumi imara licha ya mtikisiko wa kiuchumi ulioikumba dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam dr. Abassi amesema tafiti za mashirika mbalimbali ya kimataifa zimethibitisha kuwa uchumi wa tanzania unakuwa kwa kasi kuliko nchi nyengine za ukanda wa afrika mashariki.


Amesema uimara wa uchumi wa tanzania haupo kwa lengo la kusifiwa na taasisi za kimataifa bali serikali imeweza kutekeleza majukumu yake na kumudu kuongeza bajeti katika miradi ya maendeleo ikiwemo elimu, afya, miundo mbinu na nishati.

Aidha, amewahimiza watanzania kuachana na siasa na kuendelea kuchapa kazi, kuwa wazalendo kwa nchi yao na kuisaidia serikali katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.
chanzo:Zbc.

Comments