Marubani wa shirika la ndege la serikali nchini Algeria wamefukuzwa kazi baada ya kumruhusu mtoto yatima mwenye umri wa miaka kumi kuendesha ndege ya abiria.
Mtandao wa Africa News umesema zoezi hilo lilifadhiliwa na kurekodiwa na runinga ya El Bilad TV, waliomuonesha mtoto huyo akiwa amevaa sare za rubani akibofya vitufe katika chumba cha rubani.
Haijulikani ni abiria wangapi walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Air Algerie kutoka mji wa Algiers hadi mji Setif.
Mtandao huo unasema kuwa rubani hao wawili walifukuzwa tarehe 29 mwezi Julai huku uchunguzi zaidi ukifanywa kwa sababu kitendo hicho kilikiuka sheria za usafiri wa ndege.
chanzo:zanzibar24.
Comments