
Maalim Seif alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho Wilaya ya Magharibi A, Unguja.
“Juzi nasikia wamejaza meli ya Mapinduzi II. Kulikuwa na
mkutano wa wananchi waliokuwa nje ya nchi, nadhani ni Dayaspora.
Kulikuwa na mkutano uliofunguliwa na January Makamba kwa niaba ya Makamu
wa Rais.
Jioni yake wakatiwa kwenye meli eti wanatembezwa kwenye
visiwa mpaka mkondo wa Nungwi, meli ikasimama kwa saa mbili, ndani kuna
kamati ya ufundi iliyoundwa na watu kutoka Naijeria, Sumbawanga, Pemba
na Unguja, kumbe wanafanya kazi zao huku wanasema Dayaspora,” alisema Seif.
“Waganga hao wamepewa kazi nyingine, kuhakikisha
wanamwondoa Maalim Seif duniani na nimeambiwa na wahusika wenyewe.
Kwahiyo wenzetu kwa sasa wako hamkani hasa wakizingatia nilitoa miezi
mitatu, sijui imebaki siku ngapi sasa.”
Aliwaambia wajumbe hao kuwa katika kipindi hiki watashuhudia mambo
mengi ya kuzuia haki yao isipatikane lakini nguzo yao ni Mwenyezi Mungu
kwakuwa hawana njia nyingine.
“Ukisimama kwenye nguzo ya Mwenyezi Mungu huwezi
kuanguka. Wengine mna wasiwasi Mahakama iko upande wa Lipumba.
Ninawaambia Mahakama haipo upande wowote, inatenda haki.
“Chama chetu sasa hivi kinapita katika kipindi kigumu.
Kuna hujuma za Lipumba na genge lake ambao wote tunajua nyuma yake ni
dola na ninyi ni mashahidi jinsi gani dola inavyomuunga mkono,” alisema Seif.
chanzo: zanzibar24.
Comments