Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvi amesema mtu
yoyote asiyelipa kodi ya ardhi na kuendeleza ardhi hiyo, ni sababu
tosha ya kunyang'anywa ardhi hiyo pamoja na kufutiwa hati ya umiliki kwa
kuwa anaingizia hasara serikali
Waziri
Lukuvi amebainisha hayo ikiwa imepita siku moja tokea kwa aliyekuwa
Waziri Mkuu wa awamu ya tatu, Mh. Fredrick Sumaye kudai chanzo cha
kupokonywa shamba lake ni siasa tu za yeye kuhama chama cha CCM na
kwenda kuupa nguvu upinzani.
Akiongea kuhusu mashamba na viwanja kuchukuliwa Waziri Lukuvi amesema,
"Kila
mtu atambue iwe ni kiwanja au shamba kama unatabia ya kutolipa kodi ya
ardhi ni sababu tosha ya wewe kunyang'anywa shamba lako au ardhi
unayomiliki.
"Imejitokeza
kwa watu wachache kuchukua ardhi kubwa kwa miaka mingi kuliko hata
uwiano wa uendelezaji wa ardhi hiyo, kwa mfano kuna hati moja hapa
ambayo inapigiwa kelele tokea mwaka 1939 imekuwa ikitembea mikono mwa
watu. Sasa miaka ile watu walikuwa wachache unapokwenda kuchukua ardhi
ya kijiji hekari elfu 60 kwa mfano hivi sasa wananchi utakuwa umewaachia
kitu gani?" Amesema Lukuvi
Pia
Waziri Lukuvi amesema imekuwa kawaida ya baadhi ya watu wanapowahi
maeneo huwa wanakimbilia kuchukua sehemu zenye manufaa makubwa kwa
upande wao na mwishowe wanashindwa kuendelezaa maeneo hayo kama
walivyoyakimbilia.
"Unawahi
kuchukua sehemu zenye manufaa kama mto, ardhi inayolimika, sasa
unachukua hekari zote hizo halafu huliendelezi mwishowe shamba hilo hilo
tunalikuta Benki umelikopea fedha.
Kisha umepata fedha hizo unakwenda
kujengea 'apartment' sehemu nyingine na kule wananchi wanalimezea
mate.Serikali wanatumia nguvu kubwa sana kutuliza wananchi wasivamie
hilo shamba , halilimwi, serikali hatupati kodi", alisisitiza Lukuvi.
Kwa
upande mwingine, Waziri Lukuvi amesema serikali imekuwa na huruma kwa
miaka mingi kwa wananchi wake lakini serikali ya uongozi huu
wamekubaliana kila mtu afuate sheria anazo paswa
chanzo:mpekuziblog.
Comments