Wafugaji wa nyuki Zanzibar kwa kushirikiana na jumuia yao (ZABA) wameandaa siku ya nyuki ambayo itakayofanyika leo tarehe 22 August 2017 huko Makunduchi Mkoa wa Kusi Unguja.
Akizungumza na Zanziba24 Mwanaharakati wa Mazingira Ishaka Hussein Abdallah amesema kuwa tukio hili ni la mara yakwanza kufanyika kwa kuadhimisha siku ya nyuki Zanzibar ,pia kutakuwa na maonyesho mbalimbali ambayo yatakayo jumuisha bidhaa za nyuki pamoja na kujua umuhimu wake.

Asali
Hata hivyo amefahamisha kuwa ufugaji wa Nyuki unafaida nyingi kwa jamii ikiwemo kulinda misitu isipotee kwani nyuki hufugwa sehemu yenye msitu, pia nyuki husaidia huzalisha vyakula kwamfano nyuki anapo tembelea mauwa ya matunda anajenga uwezekano mzuri wa kukua tunda hilo, na pia asali yake ni tiba kwa Mwanaadamu.
Mwanaharakati huyo amesema siku hiyo ni adhimu kwani watahudhuria watu wengi mashuhuri akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Idrisa Muslim Hijja.
chanzo:zanzibar24.
Comments