Mbunge
wa Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema amewageukia viongozi wa dini
nchini kwa kusema kwamba wanapaswa kukemea vitendo vya udhalilishwaji
wanavyofanyiwa wabunge wa upinzani na siyo kukemea viroba na bia.
Lema
aliitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari Mjini Arusha na
kusema kuwa viongozi wa dini mbalimbali nchini wasifumbe macho yao na
kujifanya hawayaoni mateso wanayopatiwa viongozi wa upinzani nchini.
"Viongozi
wetu wa dini wasijifanye hili tunalofanyiwa upinzani hawayaoni. Kazi ya
viongozi wa dini siyo kukemea bia na viroba bali wanatakiwa wapige
kelele kwenye ukiukwaji wa misingi ya sheria inayoendelea hapa nchini
dhidi ya upinzani", alisema Lema.
Pamoja
na hayo, Mhe. Lema ameongeza kuwa viongozi wa dini endapo watasimama
katika kukemea maovu yanayofanywa ndani ya nchi yakiwepo ya unyanyasaji
watakuwa wamelikomboa taifa kwenye machafuko.
"Ipo
siku kuna watu watashindwa kuvumiliwa haya tunayofanyiwa, hapo ndipo
vita vya wenyewe kwa wenyewe vitakapokuja hapo siku za mbeleni" alimaliza.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments