Kuimarisha mazingira ya utoaji wa elimu kwa njia ya teknologia.

Wizara ya elimu na mafunzo ya amali imeshauriwa kuimarisha mazingira ya utoaji wa elimu kwa njia ya teknologia ili kurahisisha ufundishaji wa masomo ya sayansi na hisabati.

Afisa wa shirika la kimataifa la elimu unesco mathias luhanya amesema hivi sasa dunia inakwenda na kasi ya maendeleo ya teknolojia hivyo kunahitajika ubunifu mkubwa katika kufikia malengo ya elimu.


Akizungumza katika mkutano wa kujadili lengo la nne la mpango wa millenia kuhusu elimu amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ya mapinduzi zanzibar ili kuhakikisha zanzibar inatoa elimu bora.

Katibu mkuu wizara ya elimu mafunzo ya amali khadija bakari amesema serikali inaendelea kuimarisha mpango wa elimu wa awamu ya pili zanzibar kwa kuzingatia vigezo na miomgozo ya kimataifa ili uweze kukidhi mahitaji ya mabadiliko ya teknologia.
chanzo:Zbc.

Comments