Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana amefunguka
na kusema kuwa anachofanya Rais Magufuli ni sawa kwani yeye ana
sahihisha makosa ambayo yalifanywa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) waliopita.
Kinana
amesema hayo jana alipokuwa akiwasalimia wananchi katika kijiji cha
Mkanyageni wilayani Muheza katika ziara ya kikazi ya Rais Magufuli
mkoani Tanga iliyoanza jana mpaka siku ya Jumamosi ambapo Rais ataweka
jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini
Uganda mpaka Chongoleani Tanga.
"Yako
maneno yanayosema kwamba wakati mwingine Rais Magufuli ni mkali, wakati
mwingine wanasema Rais anakosoa awamu zilizopita, awamu zote zilizopita
ni za CCM awamu hii ni ya CCM kama kuna kasoro, au kama kuna mambo
awamu zilizopita hayakwenda vizuri awamu hii ya CCM chini ya Magufuli
kukosoa au kusahihisha yale yaliyoharibika huko nyuma si dhambi.
Aliyeharibu Mwana CCM, anayekosoa mwana CCM na anayesahihisha ni mwana
CCM tuache kulalamika tuchape kazi" alisema Kinana
Mbali
na hilo Kinana amesema wanachotaka wananchi ni maendeleo na ndiyo kitu
ambacho Rais Magufuli anafanya sasa na kudai yeye anatimiza mahitaji ya
wananchi na kufanya yale mambo ambayo viongozi wengine walikuwa
hawafanyi.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments