Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wametoa tamko lao baada ya jeshi
la polisi kuzuia kongamano lililotakiwa kufanyika kumuenzi aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama hicho, Alphonce Mawazo mkoani Geita.
Mmoja
wa wanachama wa Chadema, Dr. Mussa Mdede ambaye pia katika kongamano
hilo alikuwa mmoja kati ya watoa mada, amesema kitendo hiko cha polisi
kuzuia Kongamano ni kitendo kinyume na sheria Namba 5 ya Vyama vya Siasa
ya Mwaka 1995.
”Jeshi la polisi linahitajika kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mikutano ya hadhara ndivyo sheria inavyosema”. amesema Mdede.
”
Kongamano ambalo limezuiwa ni shughuli ya ndani ambayo kimsingi sheria
ya vyama vya siasa inatulinda. Kimsingi ni kongamano ambalo lilikuwa
halali na tunapofanya kongamano la ndani hatuhitaji ulinzii wa jeshi la
polisi” amesema Mussa Mdede.
Hivyo
Mdede amemuomba mkuu wa jeshi la polisi nchini, IGP Simon Sirro kutumia
nafasi yake kuwakumbusha polisi majukumu yao kwani kwa sasa anaona
wanafanya kazi kwa mwamko wa kisiasa.
"Chadema
tunasema, kwanza tunamwambia IGP Simon Sirro kwamba awakumbushe Askari
wake kufanya kazi kwa weledi wasifanye kazi kwa kisiasa. Katika awamu
hii ya tano jeshi la polisi limekuwa likifanya siasa waziwazi.” Mussa
Mdede.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments