Chama
cha ACT Wazalendo kimeshtushwa na kauli (amri) ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, ndugu John Pombe Magufuli aliyoitoa hivi karibuni
akiwa Mkoani Tanga ya kutaka Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Mazingara,
Kata ya Mkata, Wilayani Korogwe, katika Mkoa wa Tanga ahamishwe katika
kituo hicho mara moja.
Hatua
hiyo ni baada ya malalamiko ya mkuu wa wilaya ya Korogwe, ndugu Godwin
Gondwe kuwa kesi zote kati ya wakulima na wafugaji katika mahakama hiyo
wanashinda wafugaji, na hivyo kumtuhumu hakimu huyo, aliyetajwa kwa jina
moja la Laizer kuwa anapendelea wafuagaji.
ACT
Wazalendo tunalaani kauli hii ya Rais kwa kuwa inakiuka misingi ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara 107B
ambayo inaipa Mahakama Haki na Uhuru wa kufanya kazi yake bila
kuingiliwa wala kubughudhiwa na mihimili mingine.
Katiba
inaainisha mgawanyo wa Madaraka baina ya Serikali, Mahakama na Bunge.
Kitendo cha Ndugu Rais kutaka Hakimu wa Mahakama achukuliwe hatua kwa
kuhamishwa ni kuuingilia Mhimili wa Mahakama ambao katiba na misingi ya
utawala bora inahitaji mhimili huo pamoja na wanaohudumu wawe huru na
kufanya kazi zao bila ya shinikizo la mtu yeyote iwe la kisiasa au
kijamii.
Sisi
ACT Wazalendo tunaamini kuwa hata kama tuhuma dhidi ya Hakimu mhusika
ni za kweli, na kuwa ipo haja ya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake,
basi lazima utaratibu wa hatua hizo za kinidhamu kwa Hakimu huyo
ufuatwe, kwa kuchunguzwa kwanza, kupata ushahidi na akikutwa na hatia
basi achukuliwe hatua na mamlaka yake ya nidhamu, ambayo ni Tume ya
utumishi wa Mahakama. Hatuamini kama hakimu anayedaiwa kupendelea katika
kutoa hukumu anapaswa kuhamishwa tu.
Ni wazi kauli hii ya Rais inalenga kuwatia hofu Majaji na Mahakimu wengine.
Na
utekelezaji wake utaiaminisha jamii kuwa hatima za Majaji na Mahakimu
katika kazi zao zipo mikononi mwa Rais na sio utaratibu wa Sheria
uliowekwa. Amri hii ni batili, ni kinyume cha Katiba, na ikitekelezwa ni
uvunjifu wa Katiba ya Nchi!
Katika
jambo hili, ACT Wazalendo tunamtaka Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim
Juma ajitokeze hadharani kukemea amri za namna hii zinazoudogosha
mhimili wa mahakama, atoe kauli ya kuwahakikishia Mahakimu na Majaji
kuwa usalama wa majukumu yao (security for tenure) unalindwa na
utaendelea kulindwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi. Na kuwa kama
yapo malalmiko juu ya hakimu Laizer basi utaratibu ufuatwe.
ACT
Wazalendo pia inamsihi Rais kumchukulia hatua za kiutawala Mkuu wa
Wilaya ya Handeni Bwana Godwin Gondwe Kwa kumwingiza Rais kwenye mgogoro
wa kikatiba usio wa lazima. Mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa vikao vya ngazi
za chini vya michakato ya kutazama maadili ya mahakimu na anajua
taratibu za kufuata. Alichofanya Mkuu wa Wilaya ni kitendo kinachopaswa
kukemewa kwa hatua kali kuchukuliwa dhidi yake ikiwemo kumwajibisha ili
iwe fundisho kwa Wakuu wa Wilaya wengine wanaoshindwa kufanya kazi zao.
Mwisho,
tunavitaka vyama vya mawakili vya Tanganyika na Zanzibar na taasisi
nyengine zenye kupigania utawala wa Katiba na Sheria nchini kujitokeza
na kulaani kauli ya Rais na kumshinikiza Rais au kupitia waziri wake wa
Katiba kuwaomba radhi watanzania kwa jaribio hili la kutaka kuvunja
misingi ya katiba waliyoapa kuilinda.
Thomas E. Msasa
Mwenyekiti- Kamati ya Sheria na Katiba
ACT Wazalendo
Agosti 09, 2017
RAIS AACHE KUVUNJA KATIBA, HANA MAMLAKA YA
KUMUONDOA HAKIMU
Chama cha ACT Wazalendo kimeshtushwa na kauli (amri) ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu John Pombe Magufuli aliyoitoa ...
See more
KUMUONDOA HAKIMU
Chama cha ACT Wazalendo kimeshtushwa na kauli (amri) ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu John Pombe Magufuli aliyoitoa ...
See more
104
| chanzo:Mpekuziblog. |
Comments