Jaji Mkuu Zanzibar kutafuta muarobaini wa kesi zinazolalamikiwa.

Jaji Mkuu Zanzibar Mhe. Omar Othuman Makungu ameahidi kuzifuatilia kesi zote zinazo  lalamikiwa na wanafunzi vyuo vya mafunzo (mahabusu)   kisiwani pemba kuhakikisha majaji na hakimu wanazimaliza  kesi  zao katika kipindi kifupi kijacho  ili  kila mtu apate haki yake.

Jaji Makungu ameyasema hayo huko chuo cha mafunzo gereza kuu la wete kisiwani pemba wakati alipo fanya ziara ya kulitembelea kusikiliza matatizo yanayo wakabili wanafunzi katika vyuo.
Amewahakikishia kuwa tatizo la kutofikishwa mahakamani litamalizika kutokana na kwamba ameshakutana na taasisi nyengine kama polisi na kujua chanzo cha washitakiwa kutofikishwa mahakamani.
Akiwasilisha taarifa ya wanafunzi na mahabusu wa vyuo vya mafunzo  pemba kwa niaba ya wengine  huko makao makuu ya vyuo vya mafunzo  wete   Fadhil Yussuf Himid  kwa jaji mkuu wa Zanzibar wameomba kuwepo kwa jaji mkaazi  ili kuondosha matatizo hayo ikiwemo kutofikishwa mahakamani kwa wakati.
Akitoa malalamiko yao alizitaja baadhi ya kesi ambazo bado hadi leo hazijapatiwa ufumbuzi zikiwemo rufaa ambazo hazijaitwa mahakamani  na zimebakia kutolewa hukumu tangu mwaka 2015.
Kamishna wa vyuo vya mafunzo Ali Abdalla Ali amesema yapo matatizo mengi katika vyuo vya mafunzo hasa kwa  pemba ikiwemo ukosefu wa magodoro kwa wanafunzi na mahabusu.
 chanzo:zanzibar24.

Comments