Mbunge
wa Kawe, Halima Mdee kupitia kwa Mawakili wake amewasilisha pingamizi
la awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa Mahakama hiyo
haina mamlaka ya kusikiliza kesi yake ya kumtolea lugha chafu Rais
Magufuli.
Mawakili
watano wa Halima Mdee, wakiongozwa na Hekima Mwesigwa wamewasilisha
pingamizi hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya
Wakili wa Serikali Leonard Chalo kudai shauri hilo limekuja kwa ajili ya
kitajwa.
Mwesigwa
amedai kuwa wana mapingamizi mawili, kwanza hati ya mashtaka ina
mapungufu, pia Mahakama hiyo haina mamlaka akisema kuwa Mahakama hiyo
haina mamlaka kwa sababu, Mkuu wa Wilaya aliyetoa amri ya kukamatwa kwa
Mdee ameshindwa kufuata matakwa ya kisheria.
Baada ya kueleza hayo kesi hiyo imeahirishwa hadi September 12, 2017.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments