Halima Mdee atoa malalamiko juu ya Jeshi la polisi.

Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Halima Mdee amefunguka na kusikitishwa na jeshi la polisi kushindwa kuwakamata matapeli ambao wamekuwa wakitapeli wananchi kwenye mitandao kupitia jina lake.


Amesema kuwa ni muda mrefu alishatoa taarifa kwenye jeshi la polisi kuhusu watu hao wanaotumia jina lake kwenye mitandao ya kijamii na kujifanya kutoa mikopo yenye riba ndogo na kuwatapeli wananchi pesa zao.

“Wanaojitambulisha kutoa mkopo kwa jina langu ni matapeli, sihusiki nao !Nimetoa taarifa polisi inaonekana hawakamatiki” alisema Halima Mdee
chanzo: zanzibar24.

Comments