Mbunge
wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya (Chadema) amelazwa katika Hospitali
ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua
ghafla akiwa rumande ambako alikuwa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi
Kanda ya Tarime Rorya baada ya kumkamata akiwa hotelini kwa madai ya
kutaka kufanya mkusanyiko usio halali.
Taarifa
za kulazwa kwa Bulaya zimethibitishwa na Mbunge wa viti maalumu mkoa
wa Mara Joyce Sokombi (CHADEMA) ambapo amezungumzia hali ya Mbunge huyo
kwa sasa, na kusema kwamba hali yake bado haijatengemaa kwani amepewa
rufaa kwenda hospitali ya mkoa.
Mh.
Sokombi amesema presha ya Ester Bulaya bado ipo chini, kiasi kwamba
wameshindwa kumsafirisha kwenda hospitali kubwa, hivyo wanasubiri
madaktari wamsaidie kurudisha hali ya presha yake, ndipo wamtoe
hospitali.
Pia Mh. Sokombi amesema kwa sasa Bulaya ameshapatiwa dhamana akiwa hapo hospitalini.
Pia Mh. Sokombi amesema kwa sasa Bulaya ameshapatiwa dhamana akiwa hapo hospitalini.
chanzo:mpekuziblog.
Comments