Dk shein atilia mkazo ujenzi wa barabara ya Magogoni –Kinuni.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Muhammed Shein amewaagiza wajenzi na wasisimamizi wa barabara ya Magogoni –Kinuni kuimaliza Barabara hiyo mpaka kijito upele ili kuwaondoshea usumbufu wananchi wakati wakihitaji huduma ya usafiri.

Akizungumza katika ukaguzi wa barabara hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika Mkoa wa Mjini Magharib Unguja,Dk.Shein amesema kutokana na wananchi kuwa na mahitaji makubwa ya barabara hiyo hususani kinamama wajawazito ni vyema kujengwa kama ilivyo kusudia na kumaliziwa kipande kilichobaki.
Akizungumzia suala la usalama wa barabarani  Dk.Shein amesema mbali na barabara hiyo kujengwa kwa kufuata sheria za ujenzi ikiwemo kuwekwa kwa alama za barabarani lakini jeshi la polisi lina wajibu kusimamia ipasavyo sheria za barabara ili kuwachukulia hatua za kisheria wavunjifu wa Sheria za barabara.
Aidha Dk Shein amesema kutokana na kuripotiwa kwa kesi nyingi za uvunjaji wa sheria za Barabarani wakati umefika kwa wasimamizi wa sheria hizo kufanya kazi kwa uadilifu ili kupunguza ajali zinazoendelea kujitokeza ambazo husababisha hasara na Vifo kwa watumiaji wa barabara.
Nae Naibu katibu Mkuu wa ofisi wa Raisi ,Tawala za Mikoa na Idara Maaalumu za SMZ, Radhia Rashid amesema kukamilika kwa Ujenzi huo kutasaidia kupunguza tatizo la usafiri linalowakabili wananchi kwa muda mrefu na kutowa wito kwa wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari kwa watoto kutokana na barabara hiyo kuwa karibu na makaazi ya watu.
Jumala ya shilingi million 1.2 zimetengwa kwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo ina urefu wa kilomita 3.6-2 ambapo kwa awali itajengwa kwa urefu wa mita 2.1-5 chini ya kampuni ya MECO.
chanzo:zanzibar24.

Comments