Mbunge wa jimbo hilo mhe: juma othman haji amesema wataalamu hao watashirikiana na wa mamalaka ya maji zanzibar zawa ili kufanikisha kurejea huduma hiyo haraka kwa wananchi.
Amewataka wakaazi wa jimbo hilo kuwa na ustamilivu wa usumbufu wa uhaba wa maji safi na salama katika jimbo hilo kwani mbunge huyo na mwakilishi wapo mbioni kulitatua tatizo hilo.
Akizungumza mara baada ya kukagua visima vitatu katika jimbo hilo vilivyojengwa kwa kushirikiana na mbunge na mwakilishi wa jimbo la tumbatu mhe: juma amesema anatambua kuwepo na changamoto ya uhaba wa maji safi na salama kwa baadhi ya wakaazi wa jimbo hivyo wanatarajia kuliondoa katika kipindi hiki cha karibuni ili kutimiza malengo ya serikali zote mbili za kuwasogezea huduma za kijamii wananchi wake.
Amesema ameamua kuchukuwa wakandarasi kutoka dawasa wakishirikiana na wakandarasi wa mamlaka ya maji zanzibar (zawa) ili kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa haraka zaidi na kuwaondolea usumbufu wakaazi hao.
Aae mkandarasi wa dawasa archard mutalemwa amesema visima walivyo vikagua vinamaji mengi sana hivyo kukamilika kwake vinaweza kuondosha uhaba wa maji safi na salama katika jimbo la tumbatu na ameahidi kukamilisha mradi huo kama ilivyo pangwa ili wananchi waipate huduma hiyo ipasavyo.
Awa upande wake mkaazi wa jimbo hilo ali jega amemshukuru mbunge huyo kwa kushughulikia tatizo la maji safi na salama kwani walikuwa wakitumia maji yasiyo kuwa salama kwa kipindi kirefu hivyo kufanikisha kupatikana maji kwa visima hivyo kutawaondolea usumbusu huo.
Visima alivyokagua mbunge huyo ni kisima cha kipange,kisima cha mwanzo mgumu pamoja na kisima cha mzimni.
chanzo:Zbc.
Comments