Chama cha CUF Kisiwani Pemba yaunga mkono maadhimio ya bara kuu.



CHAMA CHA WANANCHI CUF Kisiwani Pemba kimeendelea kuunga mkono maamuzi yote yaliyo chukuliwa na Baraza Kuu la Uwongozi  Taifa lililo kutana na kutoa maamuzi tarehe 28/07/2017 VUGA mjini Unguja  kuhusiana na hujuma za dola dhidi ya chama hicho.

Akitoa taarifa kwa vyomba mbali mbali vya habari Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Chake chake Nd Saleh Nassor Juma kwa niaba ya kaimu katibu wa Wakilishi na Madiwani Pemba nd. Mohammed Ali Salim amesema ni ukweli usio fichika kuwa baadhi ya vyombo vya dola vinatumika vibaya kwa chuki za kisiasa dhidi ya wafuasi wa chama hicho.


Amesema kuwa maadhimio hayo siyo tu kuwa yameweka msimamo wa chama kuhusiana na kadhiya iliyo tayarishwa na serekali zilizopo madarakani  yakueleza hujuma dhidi ya vyama vya CUF, CHADEMA  na vile vyote vilivyo undwa na ukawa.

Katika taarifa hiyo ya wawakilishi na madiwani wa CUF kwa vyombo vya habari imelaani hujuma hizo na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono  na viongozi  wa ngazi zote ndani ya  chama hicho hadi pale ushindi wao utakapo patikana.

Aidha wameahidi kuwaunga mkono  wambuge wanane na madiwani wawili ambao waliovuliwa uwanachama na mwenyekiti wa chama hicho anaetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa Ibrahim Lipumba  pamoja na wenzake kuendelea kuwatambuni kama wanavyo tambuliwa na baraza kuu la CUF Taifa kuwa bado ni viongozi halili na wapambanaji ndani ya chama hicho.

Hatahivyo wamewapongeza wabunge hao pamoja na madiwani kwa ujasiri pamoja na ukakamavu waliounyesha katika mapambano hayo kwani wanaamini yakwamba ushindi ndani ya chama hicho utapatikana hivi karibuni.

‘‘sisi hawa kwetu ni wabunge pamoja na madiwani halili wa chama chetu bali tunahawesabau kama MAKAMANDA  MADHUBUTI na MAKINI katika mapambano haya na sisi tunaahidi kuwa nao beka kwa beka ''.

Pamoja nahayo ameeleza kuwa kitendo cha spika wa bunge la Jamhuri ya muungano Mh. Job Ndugai  kufanya maamuzi ya kuwafukuza wabunge hao ni kitendo kisicho zingatia sheria wala  ustahamilivu nakuonesha udhaifu mkubwa juu ya uwongozi wake huku wakiendelea kutupia lawama kwa tume ya uchaguzi ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa nayo imeshiriki katika kukihujumu chama hicho.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua juu ya mustakbali na mwelekeo wa chama hicho Mwenyekiti wa chama cha CUF Wilaya ya micheweni Nd. Rashid Khalid Salim amesema nguvu za umma ndizo zitakazo amua juu ya mwelekeo wa chama hicho endapo juhudi za kidiplomasia hazito fanikiwa.

Comments