
Alisema makundi yanayojipanga wakati huu ambapo kwa sasa Taifa
linatarajia Wananchi waongeze nguvu zao
katika uzalishaji kwenye miradi
ya maendeleo kamwe hayatamsaidia Kiongozi atakayechaguliwa wakati
ukifika wa Uchaguzi Mkuu kuongoza Dola.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa wito huo wakati akizungumza na Viongozi
wa Chama cha Mapinduzi wa Mikoa Miwili ya Pemba ngazi ya Wenyeviti,
Makatibu na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM hapo katika
Ukumbi wa Mikutano wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
Alionya kwamba Chama katika Uongozi wa Ngazi ya Juu kimejipanga
kuwaondoa kwenye mchakato wa kuwania Uongozi wanachama wote
watakaoendeleza tabia hiyo mbaya inayozalisha Viongozi Matapeli na wasio
na uwezo wa kuongoza.
Balozi Seif alisema wakati umefika kwa Viongozi kuacha tabia ya
kupakana matope na badala yake wawaachie Wanachama wenyewe kuamua
kumpendekeza na hatimae kumchagua Mwanachama watakayehisi ana uwezo na
uzalendo wa kuwatumikia.
Alitahadharisha kwamba makundi yanayodhoofisha nguvu za Chama
yanapaswa kuelewa kwamba yanahatarisha uhai wa Chama sambamba na
kutishia Amani ya Taifa baada ya kukosa utulivu utakaosababishwa na
sintofahamu baina ya makundi hayo.
Balozi Seif aliwapongeza Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwa hatua
nzuri waliyofikia katika uendeshaji wa Uchaguzi wa ndani na kuwataka
kutumia busara, hekima na utulivu katika chaguzi za ngazi ngenine za
Chama hicho.
Aliwashauri wanachama hao kuzingatia kwa makini Viongozi
watakaowateuwa wanawavusha vyema na kuepuka kasoro nyingi zilizojitokeza
za kukaribisha baadhi ya Wapinzani kujipenyeza kwenye Mikutano na
Kamati za Chama hicho.
Balozi Seif alionyesha masikitiko yake kutokana na tabia zilizowahi
kujitokeza zilizoashiria mmong’onyoko wa ukosefu wa siri za Vikao vya
Chama hicho ambazo zilitolewa na wapinzani hao.
Akizungumzia kuhusu suala la Zao la Karafuu lilioanza kupea wakati
huu Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
aliwaagiza Viongozi wa Serikali Mikoa na Wilaya kwa kushirikiana na
Vikosi vya Ulinzi kutaifisha mali na vyombo vyote vitakavyokamatwa
kuhusika na Magendo ya zao la Karafuu.
Alisema zipo dalili za wazi za hujuma dhidi ya zao la Karafuu
zinazoendelea kufanywa na baadhi ya Watu kwa kulisafirisha zao hilo na
kuliuza Nchi jirani wakati Serikali Kuu tayari imeshaongeza Bei mara
dufu ya zao hilo na kukidhi soko lililopo.
Mapema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Kaskazini Pemba ambae
pia ni Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kusini Pemba Mzee Mberwa Hamad
Mberwa alisema Wanachama na Wananchi Mikoani na Wilayani wanaridhika na
kasi ya Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya CCM YA Mwaka 2015 –
2020.
Mzee Mberwa alisema kasi hiyo imeongeza ari kwa wanachama hao pamoja
na kutoa matumaini waliyoyatarajia wakati wa kuwamua kukipadhamana chama
hicho katika kuongoza Dola Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa Kaskazini Pemba alimuhakikishia Mjumbe
huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chanma cha Mapinduzi
kwamba Wana CCM bado wanaimani na chama chao na daima wataendelea
kukiunga mkono katika adha ya chama hicho ya kuongoza Dola kila baada ya
Uchaguzi Mkuu.
Balozi Seif amemaliza ziara yake ya siku mbili Kisiwani Pemba
kuangalia harakati za Maendeleo sambamba na kuimarisha uhai wa Chama cha
Mapinduzi akiwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya
Chama cha Mapinduzi.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
![]() |
![]() |
![]() |
Comments