Mahakama
Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017 imetupilia
mbali pingamizi la Wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofutwa uanachama na
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba ya kutaka
wabunge wateule 8 wasiapishwe na Bunge.
Uamuzi
huo, umetolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambaye amesema ametupilia mbali
pingamizi hilo la zuio la kuapishwa kwa Wabunge hao 8 na kwa mantiki
hiyo, Wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao wanaweza kuapishwa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments