Bodi
ya korosho Tanzania imeongeza vituo vya ugawaji pembejeo ili
kuharakisha usambazaji na kuhakikisha kila mkulima anapata pembejeo kwa
wakati katika kudhibiti kuenea kwa magonjwa na wadudu wanaoshambulia zao
la korosho.
Akitolea
ufafanuzi tuhuma za ucheleweshwaji wa madawa na viuatilifu Mwanasheria
na Katibu wa Bodi hiyo, Ugumba Kilasa amesema kuwa bado wapo ndani ya
wakati kwa kuwa matumizi ya viuatilifu huanza mara tu korosho zinapotoa
maua mwezi Juni.
Amesema
kuwa kufikia Agosti 20, 2017 usambazaji wa pembejeo kwa wakulima wote
kwa msimu mpya utakuwa umekamilika kwani tani zilizobaki kukamilisha
usambazaji kwa wakulima wote tayari zimeingia bandarini na zipo katika
taratibu za kutolewa ili kusambazwa.
“Serikali
ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ilitoa uamuzi
wa kugawa bure madawa na pembejeo kwa wakulima wa zao la korosho kwa
lengo la kumwezesha mkulima na kumjenga kiuchumi ili awe na uwezo wa
kujinunua mahitaji hayo kwa misimu inayofuata” amesema Kilasa
Hata
hivyo, amewaonya wale wanaotoa maneno ya kuwavunja moyo wakulima wa
zao hilo kuhusu kusambazwa kwa madawa na viuatilifu kwambi si huduma ya
bure na kusema kwamba serikali imeamua kutoa madawa hayo kwa wakulima
bure na kila mtu atapata kulingana na mgawo wa madawa hayo
chanzo:Mpekuziblog.
Comments