Auawa kwa wivu wa mapenzi.

Msichana mmoja mwenye miaka 25, Janet Mwenda anashikiliwa na Polisi mkoani Mara kwa tuhuma ya kumuua kwa kisu mpenzi wake, Mgini Aaron mwenye miaka 37.

tukio hilo amelifanya juzi saa 11 jioni katika Kitongoji cha Kitaramanka Kijiji cha Magunga Kata ya Mirwa wilayani Butiama, ambako mtuhumiwa alimchoma kisu mpenzi wake huyo katika titi la kushoto na kumsababisha kifo.

Kamanda wa Polisi wa Mara, Jafari Mohamed amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi, ambapo Janet alifika nyumbani akitoka matembezini na kuingia bafuni kuoga na ndipo mpenzi wake alipomtuhumu kwa kumsaliti huko alikotoka.

Kamanda Mohamed alisema Aaron alipoona mpenzi wake akioga, aliona si hali ya kawaida na ndipo alipoanza kumpiga kwa kudai yeye ni msaliti na ndipo mtuhumiwa alipochukua kisu na kumchoma na kusababisha kifo chake.

Mwili wa marehemu, umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa kwa uchunguzi zaidi.
chanzo:zanzibar24.

Comments