Kwa akali askari saba wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu yalilolenga msafara wa magari ya jeshi karibu na mji wa Baidoa nchini Somalia.
Kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab limetangaza kuhusika na hujuma hizo na kudai kuwa, limeua askari kadhaa wa Somalia na wengine wa Ethiopia wanaohudumu chini ya mwavuli wa Kikosi cha Kusimamia Amani cha Umoja wa Afrika nchini humo AMISOM.
Duru za polisi zimearifu kuwa, shambulizi la kwanza lililenga msafara wa magari ya jeshi uliokuwa ukitoka katika wilaya ya Wajid, jimbo la Bakol kuelekea Baidoa abapo wanajeshi wanne waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Comments