Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini
Pemba Shekhan Mohd Shekhan amesema baada ya askari akiwemo yeye
mwenyewe binafsi kuwasili eneo la tukio walimkuta huyo kijana
ameshafariki Dunia.
Akielezea zaidi juu ya tukio hilo amesema kuwa katika uchunguzi wa
awali wamebaini kuwa kijana huyo alikua ni mwizi na inaonesha
alishambuliwa na watu na yeye Marehemu alikutwa na nazi na kipolo
pamoja na matunda.
Aidha Kamanda Shekhan ameitaka jamii kutojichukulia sheria mikononi
mwao na badala yake wafuate sheria ili kuweza kuwafikisha katika vyombo
vya sheria na ni kosa la jinai kujichukulia sheria mkononi.
Kwa upande wake Daktari dhamana wa Hospitali ya Chake chake Habibu
Khamis amekiri kupokelewa mwili wa Merehemu huyo na uchunguzi
umebainisha chanzo cha cha kifo chake ni kutokana na majeraha makubwa
aliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuchomwa kitu chenye ncha kali.
Nae mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mh. Salama Mbarouk Khatib amesema
kuwa walipata taarifa ya kuonekana kwa marehemu huyo wakati wakiwa
katika maadalizi ya ziara rasmi ya Rais wa Zanzibar hapa Kisiwani Pemba.
Amefahamisha kuwa kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama
vya Mkoa wa Kusini Pemba waliweza kufika katika eneo la tukio na
kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka hospitali ya Wilaya ya
ChakeChake kwa uchunguzi baadae mwili huwo kukabidhiwa kwa ndugu wa
marehem kwa mazishi.
Comments