ZECO linamtafuta mtu ambae amefanya udanganyifu kwa kubadilisha mita za tukuza na kudai malipo.

Wananchi wametahadharishwa kuwa makini na udanganyifu unaofanywa na watu wanaojifanya wakafanyakazi wa shirika la umeme zeco kwa kutaka kuwabadilishia mita za tukuza na kudai malipo.

Afisa uhusiano wa zeco salum abdalla hassan akizungumza na zbc kuhusu kujitokeza vitendo hivyo amesema shirika linamtafuta mtu ambae ameshafanya udanganyifu huo katika maeneo kadhaa hasa ya mkoa wa kaskazini unguja kwa kuwahadaa wananchi na kujipatia fedha huku akitoa risiti zisizo halali.


Amesema kwa kushirikiana na jeshi la polisi wanafanya uchunguzi kumbaini mtu huyo na kumchukulia hatua zinazofaa huku akiwataka wananchi kufuata taratibu halali kupitia shirika la umeme pindi wanapohitaji huduma za kuungiwa umeme.

Amefahamisha kuwa shirika limejipanga kukamilisha ufungaji wa mita za tukuza kwa maeneo yaliyobakia katika kipindi cha miaka miwili .
chanzo:Zbc.

Comments