
Akizungumza na waandishi wa Habari Mjini Zanzibar katibu mkuu wa ZATU
Mussa Omar Tafurwa amesema kwa sasa walimu wamekuwa na mwamko mkubwa
wa kujiendeleza kitaaluma ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi
lakini bado wanakabiliwa na tatizo la mishahara isiozingatia kiwango cha
elimu.
Aidha amesema serikali imetekeleza azma yake ya kuengeza mishahara
kwa watumishi wa serikali lakini mishahara hiyo imekuwa ikiwanufaisha
watu wachache hususani kwa watendaji wa waliochini ya wizara ya elimu.
Hata hivyo amesema mishahara hiyo pia imesababisha baadhi ya
wafanyakazi kushushwa ngazi zao za mishahara jambo ambalo linawakosesha
kujiinua kimaendeleo na kukosa kuhudumia familia zao.
Hivi karibuni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza Viwango
maalumu vya mishahara kwa watumishi wa umma ambapo kwa sasa baadhi ya
Watumishi wanalamikia kutotolewa kwa kufuata sheria zilizopo.
chanzo:Zanzibar24.
Comments