Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema inakusudia kuimarisha sekta ya utalii kwa kuweka mawakala wao katika nchi za nje ili kufanyakazi ya kuitangaza Zanzibar katika nchi mbalimbali ili kuwavuta watalii kujanchini.
Akizungumza na Mwandishi wetu Afisa Masoko na utangazaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar Halfani Ali Mohammed amesema ili kuukuza utalii Zanzibar lazima serikali itekeleze azma yake ya kuweka wakala katika nchi mbalimbali duniani kutangaza vivutio vya utalii viliopo nchini.
Hata hivyo amesema mbali na kuwepo kwa kituo cha cha wakala katika nchi ya India kinachotangaza utalii wa Zanzibar lakini pia serikali imekusudia kufungua vituo vyengine vipya katika nchi ya China, Israel na Urusi ili kuendelea kutangaza utalii wa Zanzibar.
Aidha amesema katika hatua hizo zinazotarajiwa kuchukuliwa ametoa wito kwa wakaazi wa zanziabr kutunza na kuhifadhi maeneo ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini pamoja na kuendelea kudumisha amani na utulivu.
Zaidi ya watalii Laki tatu sabini na sita Elfu mia mbili arobaini na mbili walitembelea Zanzibar kwa mwaka 2016 huku wageni kutoka nchi za Ujerumani, Italy, Marekani na Israel wanaongoza kuitembelea Zanzibar.
chanzo:zanzibar24.
Comments