Zanzibar imeamua kuimarisha miundo mbinu ya mawasiliano.

Waziri wa ujenzi, mawasiliano na usafirishaji balozi ali abeid karume amesema zanzibar imeamua kuimarisha miundo mbinu ya mawasiliano katika juhudi za kujenga uchumi wa kisasa.

Balozi karume ameeleza hayo katika ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa mtandao wa cisco kwa vyuo vikuu vya afrika mashariki katika kempasi ya suza maruhubi.

Amesema lengo la serikali kuimarisha sekta ya mawasiliano hasa katika teknolojia ya habari ni kuhakikisha taasisi zote zinatumia teknolojia hiyo katika shughuli za kila siku kuelekea katika ulimwengu wa kwanza.


Ameipongeza cisco yenye makao makuu marekani kwa kuanzisha kituo zanzibar katika chuo kikuu cha suza ambapo vijna wengi wamekua wakisoma teknolojia ya mawasiliano ya habari.

Naibu makamu mkuu wa chuo cha suza anaeshughulikia mipango na fedha dkt. Zakia aboubakar amesema mtandao wa cisco ulioanza mwaka 2004 hapa zanzibar umetoa wataalamu wa fani tofauti za teknlojia ya habari na wanachangia katika kukuza uchumi wa zanzibar.

chanzo:Zbc.

Comments