ZAFISO watakiwa kujiunga na mfuko wa pencheni Pemba.

Image result for pemba islandMkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanajuma Majid Abdalla amewashauri wanachama wa Umoja wa wajasiriamali Zanzibar ZAFISO kujiunga na mfuko wa Pencheni wa PPF ili kujikwamua na masikini.
 
Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo alipokuwa akifungua semina ya siku moja ya wajasiriamali huko katika Ukumbi wa kiwanda cha mafuta ya makonyo wawi Kisiwani Pemba yenye lengo la kuzungumzia umuhimu wa kujiunga na mifiko ya hidha ya jamii.
 
Amesema mfuko wa pencheni wa PPF ni njia itakayo wapelekea wajasiriamali kufanyakazi kwa uhakika na mafanikio.
 
Hata Hivyo Mkuu huyo wa Mkoa amewakataka wajasiriamali hao kujitathmini ili kuweza kuzitumia fursa zilizopo kwa lengo la kupata mafanikio zaidi.
 
Chanzo: zanzibar24.

Comments