
Afrika mashariki inatarajia kujenga mradi mkubwa wa kawi katika eneo
la Stiegler Gorge ndani ya turathi za UNESCO, katika eneo la uhifadhi wa
wanyamapori la Selous kwa dhumuni la kuimarisha sekta yake ya kawi.
Shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyamapori (WWF) limeonya kuwa
njia inayotumiwa na wanyama pori wakati wanapohamia maeneo mengine ita
kabiliwa na mradi huo huku watu 200,000 wanaotegemea eneo hilo kwa
kipato wakiathiriwa na mradi huo.
Bwawa la umeme linatarajiwa kujengwa katika turathi hizo za UNESCO
lenye ukubwa wa taifa la Switzerland ambalo ni maarufu kwa wanyama
tofauti.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alisema hakuna pingamizi yoyote itakayo zuia serikali yake kujenga mradi huo.
”Naelewa kwamba mradi huu wa Stiegler Gorge utapingwa na
wengi, Utapingwa kwa sababu eti kuna maswala ya mazingira ambayo
yanapaswa jkuangaziwa na wengine watasema kwa sababu unajengwa katika
mbuga ya uhifadhi wa wanyama pori ya Selous.Mradi huu utakabiliwa na
pingamizi chungu nzima lakini nawataka raia wa Tanzania kutahabiti ili
kuhakikisha kuwa mradi huu unafanikiwa”.
Mpaka sasa Tanzania ina idadi ya watu milioni 53 ina Megawati 1400
ya umeme ambapo mradi wa bwawa hilo unakadiriwa kutoa Megawati 2000 za
umeme.
Rais amesema mradi huo utachukua asilimia 3 pekee ya eneo hilo la uhifadhi wa wanyama pori.
Shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyama pori WWF, linaitaka
serikali ya Tanzania kufanya utafiti wa kina wa mazingira katika eneo
hilo ili madhara yote yabainike kabla ya mipango ya mradi
huo unaotarajiwa kugharimu dola bilioni mbili za Marekani kuanza.
chanzo: zanzibar24.
Comments