Wizara ya Habari yapambana na Utamaduni Zanzibar.

Wizara ya Habari Utalii,Utamaduni na Michezo imesema kutokana na kupotea  kwa kiasi kikubwa  mila na utamaduni wa mzanzibar  visiwani Zanzibar  itahakikisha kupambana  na  kutoa elimu  ili utamaduni wa mzanzibari usipotee.

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari Juu ya siku ya Tamasha la mzanzibar Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Omar Hassan Omar Kingi  amesema  vijana wengi wakizanzibar  hivi sasa  wamepoteza  utamaduni wao  kwa  kuiga  mila  na tamaduni za kimaharibi jambo ambalo  limepelekea kushusha  thamani ya Zanzibar katika utamaduni wake na soko lake la utalii.


Amesema ifikapo tarehe 19 mwezi huu  kutafanyika tamasha la mzanzibari  ambalo lengo lake ni kuwashajihisha wananchi   na kuona umuhimu wa kutunza na kulinda mila,desturi na silka zao  hasa Zanzibar.

Hata hivyo amesema Serikali  imeweka mikakati imara  kuhakikisha   inalinda utamaduni wa mzanzibar licha ya kuwa  na  muingiliano wa wageni  mbalimbali kuja zanziabri watahakikisha  wanakuza Nyanja za utamaduni ili ziende  sambamba na sekta ya utalii ili kukuza mapato ya taifa, kuwapa kipaombele  wasanii pamoja na wazalishaji  wa vitu vya utamaduni.

Maadhimisho hayo ya tamasha la Mzanzibar yanatarajiwa kufanyika ifikapo  tarehe 19 mwezi huu katika viwanja vya mnara wa kumbumbu kisonge na kufunguliwa na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi ambapo ujumbe wa mwaka huu ni Tulinde  maadili  yetu  kupinga udhalilishaji.
Chanzo:Zanzibar24

Comments